1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais mteule wa Liberia Joseph Boakai ametoa wito wa amani

23 Novemba 2023

Rais mteule wa Liberia Joseph Boakai ametoa wito wa amani ili kuijenga upya nchi hiyo, wakati akitoa hotuba yake ya kwanza tangu alipopata ushindi mwembamba katika duru ya pili ya uchaguzi.

Joseph Boakai
Picha: Carielle Doe/REUTERS

Boakai amewahimiza Waliberia wote, bila kujali asili yao, nchi, kabila au ufuasi wa vyama vya siasa, kuungana katika safari ya kuiokoa nchi yao. Aliahidi kusambaza maendeleo kote nchini, na hasa ujenzi wa barabara kusini mashariki mwa nchi, jimbo ambalo alisema limepuuzwa kwa miaka mingi. Boakai, mwanasiasa mkongwe mwenye umri wa miaka 78, alimpiku rais wa sasa George Weah na tofauti ya kura 20,567 pekee. Weah alipongezwa na wengi kwa kukiri mara moja kushindwa na kukubali kukabidhi madaraka kwa njia ya amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW