1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Idadi ya vifo vya mafuriko nchini Libya yafikia 11,300

17 Septemba 2023

Umoja wa Mataifa umesema vifo vilivyosababishwa na mafuriko katika mji wa Derna nchini Libya vimeongezeka na kufikia 11,300.

Picha ikionyesha sehemu ya mji wa Derna ulioathiriwa pakubwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa. Picha hii ilipigwa Septemba 17, 2023
Picha ikionyesha sehemu ya mji wa Derna ulioathiriwa pakubwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa. Picha hii ilipigwa Septemba 17, 2023Picha: Hamza Turkia/Xinhua/IMAGO

Takwimu hizi zimeripotiwa leo na Ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinaadamu ya umoja huo, OCHA. Ofisi hiyo aidha imesema watu wengine 10,100 bado hawajulikani walipo kwenye mji huo ulioathirika zaidi.

Kulingana na OCHA, karibu watu 170 wamekufa katika maeneo mengine mashariki mwa Libya.

Kulingana na OCHA, iliyohusisha takwimu hizo na Shirika la misaada la Hilali Nyekundu nchini Libya idadi hiyo inaweza kuongezeka wakati shughuli za uokozi zikiendelea.

Hata hivyo, msemaji wa Hilali Nyekundu Tawfiq al-Shukri amezikana takwimu hizo na kusema idadi halisi hutangazwa na idara zilizoruhusiwa na mamlaka za Libya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW