1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya kuteketeza silaha zake za kuangamiza

20 Desemba 2003
TRIPLOS: Libya inataka kuteketeza silaha zake zote za kuangamiza na kufunga miradi yake yote ya kuunda silaha kama hizi. Taarifa hiyo ilitangazwa na Rais George Bush wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair baada ya kufanyika mapatano ya kisiri yaliyodumu miezi tisa pamoja na Marekani na Uingereza. Pamoja na hayo, wakaguzi wa silaha wa kimataifa wataruhusiwa kuingia Libya wakati wowote. Wizara ya Mambo ya Nje mjini Tripolisi ilisisitiza kuwa Libya imechukua uamuzi wa hiyari wa kuteketeza silaha za kuangamiza zinazoweza kutoa kitisho kwa usalama wa kimataifa. - Likituwama ripoti yake juu ya habari za maafisa wa Kimarekani, Shirika la Televisheni la Marekani, CCN liliarifu kuwa Libya ilikuwa na mradi wa kuunda silaha za kinyuklea. Libya tayari ina dhibiti silaha za kemikali, ikiwa pia na uwezo wa kuunda silaha za kibiolojia.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW