1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Libya magharibi, yatishia kuzuia usafirishaji mafuta

25 Juni 2023

Mkuu wa utawala wa magharibi mwa Libya, Oussama Hamad, ametishia kuzuia usafirishaji wa mafuta na gesi kutoka eneo lililo chini ya udhibiti wake,

Oil Terminal Az Zuwaytina
Picha: Maurizio Gambarini/dpa/picture alliance

Hamad ameidai serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa ya mjini Tripoli inapoteza mapato ya nishati.

Katika taraifa yake kiongozi huyo amesema kwamba "amezuia mapato ya mafuta ya mwaka 2022 "  zaidi ya dinari bilioni 130 ambazo ni karibu dola za kimarekani bilioni 27 kama hatua ya kwanza.

 Soma pia: Libya yafikia makubaliano ya mafuta na gesi na Italia

Taarifa hiyo imeeleza kwamba serikali ya mashariki mwa Libya haitambui mamlaka ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa yenye makao yake mjini Tripoli, na iko tayari kwa hatua zaidi, ikiwa ni pamoja na kuzuia mafuta, na itatafuta uamuzi wa kisheria.

Hamad ameishutumu serikali ya Tripoli kwa kupoteza fedha za nishati kwa kile alichokuitaja kuwa ni ""matumizi makubwa kupita kiasi", bila kufafanua zaidi.

Libya ni nchi yenye hifadhi kubwa zaidi ya mafuta barani Afrika, lakini imekumbwa na mzozo tangu ulipotokea uasi ulioungwa mkono na jumuiya ya kujihami ya NATO uliomuangusha aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Moamer Gadhafi mwaka 2011.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW