Libya yaanza tena kuchimba mafuta
22 Januari 2024Matangazo
Shirika la Mafuta la Taifa (NOC) lilitangaza kuondolewa kwa zuio hilo na kurejeshwa kwa uzalishaji kamili kwenye kisima cha Al-Sharara ambacho kwa kawaida huzalisha hadi mapipa 315,000 kwa siku.
Kundi la waandamanaji la Fezzan Gathering lililojikita mkoa wa Oubari lilitangaza siku ya Jumapili (Januari 21) kwamba walifikia makubaliano na NOC ya kumaliza mkwamo huo na baadaye kuchapisha taarifa ya makubaliano hayo kwenye ukurasa wa Facebook.
Kulingana na kundi hilo, wamehakikishiwa na mbabe wa kivita nchini humo, Khalifa Haftar, anayeunga mkono moja ya serikali zinazohasimiana za Libya.