1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya yapata serikali ya mpito

5 Februari 2021

Wajumbe kutoka pande zinazohasimiana nchini Libya zimemchagua waziri mkuu wa mpito na wajumbe watatu wa Baraza la Urais litakaloiongoza nchi hiyo hadi utakapofanyika uchaguzi Desemba 24 mwaka huu. 

Libyen Proteste gegen Haftar-Truppen in Tripolis
Picha: Hazem Turkia/AA/picture alliance

Wajumbe 74 wa Jukwaa la Mazungumzo ya Kisiasa nchini Libya, LDPF yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa wamemchagua mwanaharakati wa kisiasa na mfanyabiashara Mohammed Dbeibeh kuwa waizi mkuu na balozi wa zamani wa Libya nchini Ugiriki, Mohammed Menfi kuwa mkuu wa Baraza la Urais.

Uchaguzi huo unakusudia kumaliza mgawanyiko uliopo Libya ambao umedumu kwa zaidi ya miaka mitano, huku serikali mbili zinazohasimiana na makundi washirika ya wanamgambo yakiendesha maeneo tofauti ya taifa hilo la Afrika kaskazini.

Mchakato wa kupiga kura ya kuichagua serikali mpya ya mpito ulikwenda hadi raundi ya pili baada ya makundi yote kushindwa kupata wingi wa kutosha kwenye mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa, yanayolenga kusaidia kuumaliza mzozo uliodumu kwa muongo mmoja. Awali hakukua na upande wowote uliofanikiwa kushinda kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa kwenye mkutano huo unaofanyika karibu na mji wa Geneva, Uswisi.

Soma pia:

Mkutano huo unaojadili hali ya kisiasa nchini Libya umehudhuriwa na wajumbe 74 kutoka kote nchini humo, ambapo kaimu mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Stephanie Williams, anasimamia mchakato mzima.

Fayez al-Sarraj ambaye ni Waziri Mkuu wa serikali ya Libya iliyotambuliwa kimataifaPicha: Media Office of the Prime Minister/Handout/Reuters

Jukwaa la mazungumzo ya kisiasa nchini Libya, tumekusanyika hapa kuuendeleza mchakato huu na hatimaye kuziunganisha tena taasisi za serikali katika haya yote, lakini pia kufungua njia kuelekea lengo kuu ambalo ni uchaguzi wa kitaifa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Wagombea hao wote wamekubaliana kwamba kwenye uchaguzi wa urais na bunge mwezi Desemba, hawatagombea nafasi hizo, lakini pia watawateua wanawake kwa hadi asilimia 30 kushika nyadhifa ya juu serikalini.

Tangu mwaka 2015, Libya imejikuta katika mgawanyiko kati ya serikali mbili, moja iliyokuwa eneo la Mashariki na nyingine Magharibi na ambazo zinaungwa mkono na makundi kadhaa ya wanamgambo.

Aprili mwaka 2019, mbabe wa kivita Khalifa Hafter anayeungana na serikali iliyojikita eneo la mashariki alianzisha mashambulizi yaliyolenga kuudhibiti mji mkuu, Tripoli. Kampeni yake hata hivyo ilishindwa baada ya miezi 14 ya mapambanao. Mwezi Oktoba mwaka jana Umoja wa Mataifa ulizishawishi pande zote kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano na kuanzisha mchakato wa mazungumzo ya kisiasa.

AP, AFP, DPA, Reuters

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW