1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Club Brugge yatawazwa bingwa wa msimu

2 Aprili 2020

Ligi kuu ya kandanda ya Ubelgiji imehitimishwa huku mechi za kufunga msimu pia zikifutwa, bodi inayosimamia ligi hiyo imeamua.

Fußball FC Brügge Teamfoto
Picha: picture-alliance/BELGA/B. Fahy

Uamuzi huo umetokana na janga la virusi vya Corona uliosababisha kusimamishwa kwa muda kwa ligi mbalimbali za Ulaya.

Kutokana na uamuzi huo, Club Brugge imetawazwa bingwa wa msimu huu kwani klabu hiyo iko kileleni mwa jedwali ikiwa na alama 15 zaidi ya Gent inayoshikilia nafasi ya pili.

Uamuzi huo pia una maana kuwa hakuna timu yoyote ambayo itashushwa daraja la pili, lakini timu mbili za daraja la kwanza zitapandishwa katika ligi kuu nchini humo na kujumuisha timu 18 zitakazoshiriki katika ligi hiyo msimu ujao.

Ubelgiji inakuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kufanya uamuzi wa aina hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW