Ligi ya mataifa ya Ulaya, makundi yapangwa
24 Januari 2018Kikosi cha kocha Joachim Loew cha Ujerumani kimo katika kundi la kwanza la ligi hiyo ya juu kabisa , Ligi A, katika tukio la kupanga timu lililofanyika mjini Lausanne nchini Uswisi leo Jumatano (24.01.2018) kwa ajili ya mashindano hayo mapya ambayo kwa kiasi kikubwa yatakuwa badala ya michezo ya kirafiki.
Ureno itakumbana na Italia na Poland katika kundi la 3 la Ligi A wakati Ubelgiji inapambana na Uswisi na Iceland katika kundi la 2 , na Uhispania inakabana na Uingereza na Croatia katika kundi la 4 katika viwango vya juu vinne.
Michezo itafanyika kuanzia Septemba hadi Novemba mwaka huu ambapo bingwa wa jumla ataamuliwa katika michezo ya mchujo ambayo itwakutanisha washindi wanne wa ligi ya kundi A Juni 2019. Kila timu katika ligi hizo nne zitakuwa na michezo ya mchujo ili kufikia Euro 2020 kwa ajili ya mshindi wa kundi, ama timu ya juu nyingine , ambae hatapata nafasi katika fainali kupitia michezo ya mchujo.
Loew ameeleza haja ya kukutana na "timu vigogo" kabla ya kupangwa makundi hayo na huenda akavunjika moyo kuona kwamba anakutana na timu ngumu kama Ufaransa na mahasimu wao wa jadi Uholanzi, wanaotarajia kurejea katika hali ya kawaida baada ya kushindwa kufuzu kucheza katika fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Ligi ya mataifa ya Ulaya
Italia pia inatarajiwa kupata muda wa kujijenga upya baada ya kushindwa kufikia katika fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwaka huu, wakikosa fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958.Uhispania na Uingereza zinaonekana kuwa ni timu nyingine za kiwango cha juu lakini mataifa hayo yote katika ligi A watatambua kuwa , kwa kucheza michezo minne tu , huenda kutokea matokeo mabaya na kuteremshwa kwa kumaliza wakiwa wa mwisho katika kundi lao.
Watabadilishwa na washindi wanne wa ligi B ambayo inajumuisha Ireland ikikabana koo na Wales na Denmark katika kundi namba 4 na Urusi , mara baada ya kutoka katika kuwa mwenyeji wa kombe la dunia , inakumbana na Sweden na Uturuki katika kundi la 2.
Slovakia, Ukraine na Jamhuri ya Cheki inafanya kundi 1 wakati kundi la 3 lina timu za Austria , Bosnia-Herzegovina na Ireland ya kaskazini.
"Mara nyingi tumepata malalamiko kwamba timu nzuri hucheza na timu dhaifu , na sasa watacheza wenyewe," rais wa UEFA Aleksander Ceferin alisema . "Wakati huo huo , timu dhaifu sasa zina nafasi kubwa kufuzu katika mashindano makubwa." Wakosoaji hata hivyo , wamehoji kama kuna haja ya kuwa na mashindano.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae