1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lijue kundi A la michuano ya Euro 2020.

4 Juni 2021

Michuano ya Euro 2020 inaanza Juni 11, mwaka mmoja baadae, tofauti na ilivyopangwa awali kutokana na janga la virusi vya corona. Michuano hiyo itachezwa kwenye majiji 11 kote barani Ulaya.

Fußball-EM 2020 Auslosung Playoffs
Picha: picture-alliance/Keystone/S. Di Nolfi

Michuano ya Euro 2020 inaanza Juni 11, mwaka mmoja baadae, tofauti na ilivyopangwa awali kutokana na janga la virusi vya corona. Michuano hiyo itachezwa kwenye majiji 11 kote barani Ulaya, huku nusu fainali na fainali zikitarajiwa kupigwa jijini London, Uingereza.   

Italia: Miongoni mwa timu zilizopo kwenye kundi hilo ni Italia ama Azzuri. Kwa ufupi Italia imeingia mara kumi kwenye fainali za Euro, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1968. Italia ilitakiwa kusubiri kwa miongo mitano ili kunyakua kwa mara ya pili kombe hilo la Ulaya, lakini ilipata matumaini mapya kufuatia kampeni kali ya Euro 2020 chini ya kocha Roberto Mancini. Mancini aliyepewa jukumu la kukijenga upya kikosi hicho baada ya kushindwa kushiriki michuano ya kombe la dunia mwaka 2018, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60, alifanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi wakati bado akiwa na michezo miwili mkononi. Na katika mchakato huo alitengeneza rekodi ya kushinda michezo tisa mfululizo, iliyowahi kuwekwa miaka ya 1930 na kocha Vittorio Pozzo aliyekiongoza kikosi hicho kunyakua ubingwa wa dunia mara mbili kabla ya ushindi mnono wa mwaka 1982 na 2006

Italia imejizatiti chini ya kocha Roberto Mancini aliyekuja kwa lengo kuu la kukiimarisha upya baada ya kushindwa kushiriki michuano ya dunia mwaka 2018.Picha: Italy Photo Press/IPP/picture alliance

Mancini anamuona mshambuliaji wa kati Marco Verratti anayekipiga na Paris Saint Germain kama tegemeo lake, lakini amefufua nguvu mpya kwenye kikosi hicho kwa kumuongeza mlinda lango Gianluigi Donnarumma, lakini pia baada ya kufikia fainali za michuano ya Nations League zinazotarajiwa kuchezwa baadaye mwaka huu. 

Uswisi: Kikosi kingine kinachoshiriki kutoka kundi A ni Uswisi. Kikosi hiki kimeingia mara tano kwenye fainali za kombe la Euro. Uswisi ni moja ya kikosi thabiti ambacho kimeshiriki fainali zote kubwa kasoro moja tu tangu mwaka 2004. Lakini katika nyakati hizo, hawakufanikiwa kufikia hatua ya 16 bora, na walifikia kujiona kama wasio na bahari baada ya kupoteza kwenye mikwaju ya penati dhidi ya Poland mwaka 2016. Walifanikiwa kufika fainali za kombe la Euro mwaka 2019, na tegemeo lao kubwa linabaki kwa Xherdan Shaqiri, mshambuliaji nyota anayekipiga na Liverpool, iwapo atakuwa sawa, Haris Seferovic, aliyewahi kunyakua ubingwa wa ligi ya Ureno akiwa na Benfica pamoja na Granit Xhaka wa Arsenal. Kikosi hicho kinataka kujiimarisha zaidi kwenye michuano hii, badala ya kuonekana tu wakishiriki.

Uturuki: Uturuki nayo ipo kwenye kundi A ya michuano ya Euro 2020 baada ya kushiriki mara tano. Uturuki ilifanikiwa kulipiza kisasi dhidi ya Iceland, ilipolipiku taifa hilo la kisiwa kwa kupata tiketi ya moja kwa moja ya kufuzu baada ya kutupwa nje na nchi hiyo katika mechi ya kufuzu kombel la dunia mwaka 2018, lakini droo ya nyumbani na ushindi mnono wa nyumbani wa 2-0 na droo ya 1-1 dhidi ya Ufaransa iliwapa fursa nzuri ya kuingia kwenye fainali hizi. Caglar Soyuncu wa Leicester City anayeongoza safu ya ulinzi na ushambuliaji akishirikiana na Hakan Calhanoglu wa AC Milan, na Burak Yilmaz wa Lille ya Ufaransa.

Wales ama The Dragons wanaingia mashindanoni bila ya kocha wao Ryan Giggs anayekabiliwa na kesi mahakamani.Picha: Mike Griffiths/imago images

Wales: Wales au The Dragons. Hiki ni kikosi kingine kinachoshiriki michuano ya Euro 2020 kikiwa kundi A. Wales ilikuwa timu ya mwisho kufuzu moja kwa moja kwenye michuano hii, kufuatia mchezo mzuri kabisa ulioonyesha na nyota wake Gareth Bale na Aaron Ramsey kupata ushindi dhidi ya Hungary. Kikosi hicho chenye mchanganyiko mpana, kinaamini kwamba kitakuwa kitisho kwa kila mpinzani watakaekutana naye hata kama haitakuwa rahisi kwao kurudia mfululizo wa matokeo mazuri ya kufika nusu fainali kama ilivyokuwa mwaka 2016. Wakati Bale Ramsey wakibakia nyota, wapo wengine pia mabayo wanacheza ligi kuu kwenye klabu zao za nyumbani. Wales haitakuwa na meneja wake Ryan Giggs anayekabiliwa na kesi mahakamani. Robert Page, mmoja wa wasaidizi wake aliyechukua usukani amefanikiwa kushinda mechi nne katika michezo sita, ikiwa ni pamoja na kupanda hadi kundi la nchi za juu katika mashindano ya Nations League mpaka sasa. 

Mashirika: DPAE.