Lissu aahidi mabadiliko makubwa CHADEMA
22 Januari 2025Matangazo
Lissu alichaguliwa Jumanne usiku kuwa mwenyekiti CHADEMA akimshinda Freeman Mbowe ambaye alikuwa kiongozi wa chama hicho kwa miongo miwili.
Ameanza kazi, kwa kutangaza kuwa anakwenda kumchagua Katibu Mkuu na manaibu katibu wakuu wa chama hicho katika mkutano wa baraza hilo Jumatano usiku.
Pia ametangaza nia ya kuifanyia mabadiliko katiba ya chama hicho na kuweka ukomo wa Madaraka kwa viongozi wa juu wa chama.
Soma pia: Freeman Mbowe akubali kushindwa uenyekiti CHADEMA
Lisu ameahidi kubadili mfumo wa viti maalum vya udiwani na ubunge kwa wanawake ndani ya chama hicho ili kuwepo na ufanisi katika nafasi hizo.
Matokeo ya uchaguzi huu yameibua hisia tofauti miongoni mwa wanasiasa na wachambuzi wa kada za siasa wakisema uchaguzi huu umetoa funzo.