Liverpool wameimarika licha ya kushindwa na City
9 Februari 2026
Liverpool wako pointi 4 nyuma ya Chelsea wanaoishikilia nafasi ya tano na kwa sasa wako nje ya nafasi za kushiriki Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya.
Dominik Szoboszlai aliwafungia Liverpool goli lao kupitia mkwaju wa frikiki kisha Bernardo Silva na Erling Haaland wakawapa City ushindi kwa mabao waliyoyafunga, Haaland akifunga kupitia mkwaju wa penalti.
"Mengi yametokea ambayo ni kawaida tu katika mechi hii. Tunasikitika kutopata matokeo," Slo aliliambia shirika la habari la BBC.
"Katika kipindi cha kwanza Manchester City walikuwa timu bora bila kubuni nafasi kuu ila wlaikuwa na mpira zaidi katika nusu yetu ya uwanja. Kipindi cha pili tulikuwa juu na tulikuwa na nafasi nyingi. Tumekubali mabao mengi katika muda wa ziada, na imetokea tena leo," alisema Slot.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameusifu ustahimilivu wa timu yake waliorudisha tofauti ya pointi kati yao na Arsenal kuwa sita tena.
"Ninajivunia sana tumeshinda. Kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri sana," alisema Guardiola. "Liverpool walikuwa kwenye kasi a mchezo baada ya frikiki ya Szoboszlai, sawa tu na ile aliyofunga dhidi ya Arsenal, mkwaju mzuri sana na mchezaji mzuri pia," aliongeza Guardiola.