1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liverpool yatinga fainali ya ligi ya mabingwa

4 Mei 2022

Liverpool yatinga fainali ya ligi ya mabingwa baada ya kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Villareal katika mechi yao ya nusu fainali mkondo wa pili usiku wa kuamkia leo.

Champions League I Villareal CF v Liverpool
Picha: Ian Stephen/Pro Sports Images/IMAGO

Kocha wa klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya England Liverpool, Jurgen Klopp, amesema anahisi ni kama jambo jipya kwake yeye kama kocha kufuzu kwa mara ya nne katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Champions League.

Klopp ameyasema haya baada ya Liverpool kutoka chini magoli mawili na kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Villareal katika mechi yao ya nusu fainali mkondo wa pili usiku wa kuamkia leo.

Liverpool wamefuzu kwa jumla ya magoli 5-2 baada ya kushinda 2-0 nyumbani kwao Anfield Jumatano iliyopita.

Miamba hao wa England wanaelekea mjini Paris ambapo fainali hiyo itachezwa wakiwa wanatarajia kupatana ama na Manchester City au Real Madrid ambao mechi yao ya mkumbo wa pili wataicheza usiku wa leo huko Madrid.

City walishinda mechi ya kwanza mjini Manchester kwa mabao 4-3.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW