Loew amrejesha Boateng kikosini-Wagner badala ya Gomez
29 Septemba 2017Mchezaji huyo ambaye alikuwa katika kikosi kilichotwaa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil kutoka Klabu ya Bayern ameitwa katika kikosi cha kocha Joachim Loew ambapo Oktoba 5 kitapambana na Ireland ya kaskazini na siku tatu baadaye mjini Kaiserslautern kitapambana na Azerbaijan.
Kwa upande wa ushambuliaji Sandro Wagner wa Hoffenheim atachukua nafasi ya Mario Gomez wa Wolfsburg ambaye ni majeruhi, na pia Timo Werner ameitwa kikosini. Pamoja na nahodha Manuel Neuer anakosekana pia katika kikosi hicho Sami Khedira na Mesut Ozil.
Ujerumani inaongoza kundi C ikipata ushindi mara nane kutokana na michezo minane, kwa ajili ya kufuzu kucheza katika fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi na hivi sasa inahitaji pointi moja tu katika mchezo wa Alhamis mjini Belfast dhidi ya Ireland ya kaskazini kuweza kufuzu.
Ireland inafahamu kwamba inaupungufu wa pointi tano nyuma ya Ujerumani , inahitaji mbele ya mashabiki wa nyumbani kutofungwa bao. Ireland ya kaskazini , ni ngumu katika uwanja wake wa nyumbani , amesisitiza Loew, "na hii inakuwa kitu cha kufurahisha."
Siku ya Jumapili , mabingwa hao watetezi wa kombe la dunia Ujerumani watajitupa tena uwanjani kupambana na Azerbaijan mjini Kaiserslauten.
Wachezaji walioteuliwa na kocha Loew ni pamoja na walinda mlango : Marc-Andre ter Stegen (FC Barcelona) Kevin Trapp (paris St. Germain) walinzi:
Jerome Boateng(Bayern Munich), Matthias Ginter(Borussia Moenchengladbach), Mats Hummels (Bayern Munich), Joshua kimmich (Bayern Munich) Shkodran Mustafi (FC Arsenal) Marvin Plattenhardt (Hertha BSC), Antonio Ruediger(FC Chelsea), Niklas Sule (Bayern Munich) Wachezaji wa kati/ washambuliaji Julian Brandt (Bayer Leverkusen) , Emre Can (FC Liverpool) , Jukian Draxler (Paris St. Germain) Leon Goretzka (Schalke 04) , Toni Kroos (Real Madrid), Thomas Mueller (Bayern Munich) , Sebastian Rudy (Bayern Munich ) , Leroy sane (Manchester City) , Lars Stindl (Borussia Moenchengladbach) , Sandro Wagner (1899 Hoffenheim) , Timo Werner (RB Leipzig), Amin Younes (Ajax Amsterdam)