1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Aidha Brown au Mugabe katika mkutano Ureno

21 Septemba 2007

Waziri Mkuu wa Uingerea Gordon Brown amependekeza vikwazo vipya dhidi ya Zimbabwe hapo jana na ametishia kususia mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika hapo mwezi wa Desemba iwapo Rais Robert Mugabe atahudhuria mkutano huo.

Serikali mjini Harare imesema Brown anapoteza muda wake kwa kuonya kwamba atasusia mkutano huo nchini Ureno na kusisitiza kwamba Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 83 amealikwa na kwa hiyo atahudhuria mkutano huo na arais wa nchi jirani ya Zambia amesema atausia mkutano huo iwapo Mugabe atatolewa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ureno Luis Amado baadae amesema angelipendelea Brown ahudhurie mkutano huo kuliko Mugabe lakini bado hakua mialiko iliyotolewa na kwamba atalishughukilia suala hilo katika siku chache zijazo.



Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW