1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Annan asema hali ya Iraq ni mbaya sana

4 Desemba 2006

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema hali iliopo hivi sasa nchini Iraq ni mbaya zaidi kuliko hata ile ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Akizungumza katika mahojiano na shirika la Utangazaji la Uingereza BBC ambayo yatarushwa hewani leo hii Annan ameita hali hiyo kuwa ni mbaya sana na kusema kwamba jumuiya ya kimataifa lazima isaidie kuijenga upya nchi hiyo kwa sababu hana hakika iwapo Iraq inaweza kutimiza hilo peke yake.

Amesema wakati walipokuwa na mfarakano nchini Lebanon na sehemu nyengine waliiita hali hiyo kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini kutokana na kiwango cha mauaji na chuki na jinsi makundi yanavyojiandaa kushambuliana hali hiyo ni mbaya zaida kuliko hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wiki iliopita wakati alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo Iraq iko katika vita vya wenyewe kwa wenyewe Annan ambaye muda wake unamalizika hapo Desemba 31 alisema Iraq inakaribia kabisa kuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW