LONDON : Askofu ataka Uingereza ikamn’goe Mugabe
1 Julai 2007Kiongozi mashuhuri wa kidini nchini Zimbabwe anaamini kwamba Uingereza itakuwa na haki kuvamia koloni lake la zamani ili kwamba kumn’gowa Rais Robert Mugabe.
Pius Ncube askofu mkuu wa madhehebu ya Katoliki wa Bulawayo ameliambia gazeti la Times la London kwamba kuzidi kwa ufukara nchini mwake pamoja na mamilioni ya watu kukabiliwa na njaa pamoja na kuwepo kwa kiwango kikubwa kabisa cha kupanda kwa gharama ya maisha duniani inamaanisha kwamba Uingereza itakuwa haikufanya kosa kuchukuwa hatua.
Gazeti hilo limemkariri akisema kwamba anafikiri itakuwa ni haki kwa Uingereza kuivamia Zimbabwe na kumuondowa Mugabe na kwamba wao wenyewe wangeliweza kufanya hivyo lakini kuna hofu kubwa miongoni mwa wananchi ambao yeye binafsi yuko tayari kuwaongoza.
Ncube ambaye ni mmojawapo ya wakosoaji wakali wa Mugabe amsesema rais huyo mwenye umri wa miaka 83 na ambaye amekuwa madarakani tokea mwaka 1980 amekuwa akizifanyia ubadhirifu fedha wakati wananchi wakifa njaa ametaja mfano wa hivi karibuni wa kiongozi huyo kutumia dola milioni mbili kwa zana ya kufanyia uchunguzi wakati wananchi wakiishi kwa kutegemea dola mbili kwa wiki.