1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Blair kuitisha mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya

2 Julai 2005

Uingereza imeanza kipindi cha uongozi cha miezi sita cha Urais wa Umoja wa Ulaya kwa Waziri Mkuu Tony Blair kusema kwamba ataandaa mkutano wa viongozi usio rasmi baadae mwaka huu kwa viongozi wa Ulaya kujadili mustakbali wa bara hilo.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini London akiwa pamoja na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Jose Manuel Barroso Blair amesema katika kipindi hicho cha miezi sita atalenga masuala ya kugharamia Umoja wa Ulaya pamoja na ruzuku zake za kilimo. Blair pia ameupongeza uongozi wa Barroso.

Wiki mbili zilizopita viongozi wa Umoja wa Ulaya walishindwa kukamilisha bajeti ya Umoja wa Ulaya kwa mwaka 2007 hadi mwaka mwaka 2013.Hali hiyo imetokana na kukataliwa kwa katiba ya Umoja wa Ulaya na wananchi wa Ufaransa na Uholanzi katika kura ya maoni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW