1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Blair, Schroeder na Chirac kukutana ijumaa mjini Bruxelles

10 Desemba 2003
Duru za ofisi za Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair, zimearifu Waziri mkuu huyo atakua na mkutano maalum na Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder, pamoja na Rais wa Ufaransa Jacques Chirac ijumaa ijayo mjini Bruxelles.

Mkutano huo utafanyika kabla ya kufanyika mkutano wa kilele wa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya Ulaya.

Viongozi wakuu wa Jumuia ya ulaya, wakiwemo viongozi wa nchi zilizokubaliwa uwanachama wa jumuia hiyo hivi majuzi, wote kwa pamoja wakiwa ishirini na watano, wanatazamiwa kukutana katika mji mkuu wa Ubelgiji Bruxelles, kwenye makao makuu ya Jumuia hiyo, ili kujadiliana kuhusu marekebisho ya mwisho, yatakayofanyiwa muswaada wa katiba ya jumuia hiyo.

Mkutano wa Waziri mkuu Blair, Kansela Schroeder na Rais Chirac, unaelezewa kuwa na lengo la kujadiliana kuhusu msimamo wa pamoja wa nchi hizo tatu muhimu kiuchumi katika jumuia ya umoja wa ulaya, baada ya tofauti zilizojitokeza siku za nyuma.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW