1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON ;IRA yaweka silaha chini

29 Julai 2005

Serikali za Uingereza na Ireland ya Kaskazini zimekaribisha uamuzi wa jeshi la IRA juu ya kuacha kuendesha harakati za mtutu . Hatahivyo serikali hizo zimesema uamuzi huo unapaswa kutekelezwa kwa matendo.

Lakini kiongozi wa tawi la kisiasa la IRA Sinn Fein bwana Gerry Adams amesema kwamba hatua iliyochukuliwa na jeshi la IRA itasaidia katika kuanzisha tena mazumgumzo yaliyokwama juu ya kuleta suluhisho katika mzozo wa Ireland ya Kaskazini,

Kundi la IRA jana lilitangaza rasmi uamuzi huo wa kuweka silaha chini na badala yake kutumia njia ya mazungumzo ili kutatua mzozo wa Ireland ya Kaskazini.

Kundi hilo la kikatoliki limekuwa linaendesha harakati za silaha, na kusababisha umwagaji damu mkubwa katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW