1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Je mripuko umesababishwa na bomu ndani ya barua?

6 Februari 2007

Polisi katika mji mkuu wa Uingereza,London wamesema,watu 2 wamejeruhiwa katika mripuko unaodhaniwa kuwa ulisababishwa na bomu lililofichwa ndani ya barua.Mripuko huo umetokea katika ofisi moja,kusini mwa Uingereza.Polisi waliitwa baada ya watu hao wawili kujeruhiwa kidogo katika shambulio lililotokea siku moja baada ya mwanamke mmoja kujeruhiwa mjini London na bomu lililofichwa ndani ya barua.Kwa mujibu wa polisi ni mapema mno kusema ikiwa matukio hayo mawili yanahusiana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW