1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Katiba mpya ya Umoja wa Ulaya yatumbukia mashakani

7 Juni 2005

Uingereza imeamua kuahirisha mpango wa kupigisha kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza,Jack Straw ameliambia bunge mjini London kuwa hakuna maana ya kuendelea na mipango ya kura ya maoni na hali Ufaransa na Uholanzi zimeikataa katiba hiyo.Straw amesema,hatima ya katiba mpya imetumbukia katika hali ya mashaka kwa sababu ya matokeo ya kura ya maoni nchini Ufaransa na Uholanzi.Wabunge wengine wa Uingereza wamemshauri Straw atangaze kuwa katiba hiyo imekufa,kwani kabla ya kuweza kutumika katiba hiyo inapaswa kuidhinishwa na wanachama wote 25 wa Umoja wa Ulaya.Viongozi wa Umoja huo wanatarajiwa kukutana mjini Brussels siku ya Alkhamis,kuijadili hatima ya katiba hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW