LONDON Makampuni ya Uingereza na Ulaya Mashariki yatajwa katika biashara ya silaha nchini Congo
6 Julai 2005Matangazo
Shirika la kimataifa la kupambana na rushwa, Amnesty International, limeripoti kwamba makampuni yaliyo na makao yao nchini Uingereza na Ulaya Mashariki yanasafirisha silaha kwa wingi nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Congo. Biashara hiyo inauhatarisha mpango wa kutafuta amani katika taifa hilo.
Shirika hilo limeitaka Marekani kuiwekea kikwazo cha kutouziwa silaha nchi hiyo ili kuikomesha biashara hiyo na kuitaka pia Uingereza ifanye uchunguzi. Katika ripoti yake shirika hilo limesema silaha nyingi zinapelekwa katika eneo la mashariki mwa Congo kutoka mataifa ya Balkan na Ulaya Mahariki kuchochea vita.