1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Makosa yasababisha kifo cha Mbrazil mjini London.

17 Agosti 2005

Kituo kimoja cha televisheni nchini Uingereza kimeripoti kuwa makosa kadha yamepelekea polisi wa London kumpiga risasi raia mmoja wa Brazil ambaye hakuwa na hatia ambaye alidhaniwa kuwa ni mmoja kati ya watu wanaoshambulia kwa mabomu ya kujitoa muhanga.

Jean Charles Menezes aliuwawa kwa kupigwa risasi mara nane katika kituo kimoja cha chini ya ardhi mwezi ulipita.

Polisi walikuwa wakimfuatialia kutoka katika nyumba moja ambayo ilikuwa chini ya uangalizi na ilifikiriwa kuwa inahusika katika shambulio la mabomu lililoshindwa la hapo Julai 21 mjini London.

Taarifa za mwanzo zinasema kuwa nguo za Menezes pamoja na vile alivyokuwa , viliamsha hisia za shaka shaka na kwamba hakuweza kutii amri ya polisi ya kusimama.

Lakini taarifa ya siri iliyopatikana na kituo cha televisheni cha ITV imesema kuwa picha za kiusalama zinamuonyesha Menezes kuwa hakuwa amevaa koti la baridi ambalo lingeweza kuficha bomu, na alikuwa anatembea taratibu kuelekea katika kituo hicho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW