1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Maonyesho ya muziki kuamsha uwelewa wa umaskini

2 Julai 2005

Maonyesho ya muziki jukwaani yanayowashirikisha wanamuziki mashuhuri yaliyopewa jina Live 8 yanatazamiwa kufanyika duniani kote leo hii.

Lengo la maonyesho hayo ya muziki ni kuamsha uwelewa juu ya umaskini barani Afrika na kuwashinikiza viongozi wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo ya Viwanda Duniani kuchukuwa hatua zaidi za kutokomeza umaskini.Nyota wa muziki wa Ireland na mtayarishaji wa maonyesho hayo Bon Geldof amesema maonyesho hayo ya leo yatapindukia yale ya kutafuta msaada yaliofanyika miaka 20 iliopita kuchangisha fedha kwa ajili njaa iliyokumba Ethiopia.Takriban watu bilioni tano na laki tano wanatazamiwa kuangalia maonyesho hayo kupitia televisheni ambayo yataanzia mjini Tokyo Japani.

Maonyesho hayo pia yatafanyika Berlin, London, Johannesburg na Philadelphia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW