1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

London Marathon yamuenzi Kelvin Kiptum

21 Aprili 2024

Mashindano ya mwaka huu ya mbio za London marathon yametoa heshima kwa mshindi wa mwaka jana Mkenya Kelvin Kiptum kwa dakika moja ya kupiga makofi kabla ya kuanza kwa mbio za wanaume hii leo

Kelvin Kiptum enzi za uhai wake.
Kelvin Kiptum enzi za uhai wake.Picha: Eileen T. Meslar/Chicago Tribune/AP/dpa/picture alliance

Kiptum alifariki pamoja na kocha wake katika ajali ya gari nyumbani Kenya Februari mwaka huu. Akiwa na umri wa miaka 24 tayari alikuwa bingwa wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon na alizingatiwa kuwa mshindani mkuu wa medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka huu.

Kiptum aliandika rekodi ya muda bora katika London marathon ya saa mbili, dakika moja na sekundi 25 mwaka wa 2023, huku akimaliza karibu dakika tatu mbele ya mpinzani wake wa karibu.

Video ya ushindi wake ilionyeshwa mwanzoni wa mbio za wanaume leo. Kenenisa Bekele, bingwa wa zamani wa Olimpiki Muethiopia katika mbio za mita 10,000 na 5,000 ambaye bado anashiriki katika mbio za marathon akiwa na umri wa miaka 41, alisema wiki hii kuwa Kiptum tayari alikuwa ameweka historia ya kuvutia katika mashindano hayo.