LONDON Mataifa tajiri yakosolewa kwa uuzaji silaha
22 Juni 2005Matangazo
Mataifa tajiri duniani yamelaumiwa na muungano wa kupigania haki za binadamu, kwa kuendeleza biashara ya uuzaji wa silaha, kwa serikali zinazozitumia silaha hizo kufanya vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.
Muungano huo, unaoyajumulisha mashirika ya Oxfam na Amnesty International, unasema mataifa yaliyoelendea zaidi kiviwanda duniani, G8, ikiwemo Ujerumani, yanatakiwa kuchukua dhamana kwa asilimia 80 ya silaha zinazouzwa ulimwenguni kote. Kiasi kikubwa cha silaha hizi huuziwa mataifa maskini zaidi na ambayo yameelezewa kuongoza katika ufisadi na ulaji rushwa.