London. Mawaziri wa fedha wa mataifa tajiri wakubali kufuta madeni ya nchi masikini.
11 Juni 2005Matangazo
Mawaziri wa fedha wa mataifa tajiri yenye viwanda G8 wanaokutana mjini London wanasemekana kuwa wamefikia makubaliano ya kufuta madeni ya nchi masikini duniani yanayofikia mabilioni ya Euro.
Mashirika ya habari yamewakariri maafisa wa umoja wa Ulaya na Canada katika mazungumzo hayo wakisema kuwa makubaliano yamefikiwa.
Wamesema kuwa waziri wa fedha wa Uingereza, Gordon Brown anatarajiwa kutoa maelezo zaidi juu ya makubaliano hayo hivi karibuni.
Hapo kabla , Bwana Brown amesema kuwa mawaziri hao watajadili mpango wa Uingereza na Marekani ambao unataka kufutwa mara moja deni la Euro bilioni 33 linalodaiwa mataifa 18 na benki ya dunia, shirika la fedha la kimataifa IMF na benki ya maendeleo ya Afrika ADB.