1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Mkuu wa polisi atetea kuuwawa kwa raia wa Brazil

21 Agosti 2005

Mkuu wa polisi wa jiji la London ametetea namna alivyoshughulikia tukio la kupigwa risasi na kuuwawa kwa raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 kulikofanywa na askari wake.

Ian Blair amesisitiza kwamba aliamini mtu huyo alieyeuwawa Jean Charles Mendez alikuwa mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha hadi masaa 24 baada ya mauaji hayo hapo Julai 22.Blair amesema vyombo vya habari vilikuwa vimeweka nadhari mno kwenye kupigwa risasi kwa kijana huyo badala ya miripuko ya kujitolea muhanga maisha ambayo polisi ilikuwa ikichunguza wakati ilipofanya makosa na kumuuwa Menezes kwenye treni ya chini ya ardhi.

Blair amekuja kuwa chini ya shinikizo zito baada ya nyaraka zilizovuja kutoka uchunguzi wa kesi hiyo kuonyesha kwamba polisi iliboronga na kuwekewa mashaka juu ya maelezo ya awali kutoka kwa polisi na mashahidi wa tukio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW