1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Tony awasili Uturuki.

16 Desemba 2006

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amewasili nchini Uturuki ikiwa ni kituo chake cha kwanza katika ziara yake ya mashariki ya kati yenye lengo la kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina. Blair alikuwa anatarajiwa kuwa na mazungumzo mjini Ankara na waziri mkuu wa Uturuki Recep Erdogan kujadili kujiunga kwa nchi hiyo katika umoja wa Ulaya baada ya mkutano wa umoja huo mjini Brussels. Msemaji wa Blair amesema kuwa waziri mkuu huyo atasisitiza umuhimu wa ushawishi wa Uturuki katika mataifa ya Kiislamu kitu ambacho ni sababu ya nchi hiyo kuingizwa katika umoja wa Ulaya mara itakapotimiza masharti ya uanachama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW