LONDON: Tony Blair akutana na viongozi wa kiislamu
20 Julai 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair amefanya mazungumzo na viongozi wa kiislamu nchini humo kujadili njia za kupambana na waislamu wenye itikadi kali. Kufuatia mashambulio ya mabomu mjini London hapo Julai 7 wanasiasa waislamu, viongozi wa dini na wafanyabiashara walikutana katika ofisi ya waziri mkuu Blair kwa kipindi cha saa moja.
Blair alisema baada ya mazungumzo hayo kwamba kila mtu anataka kukabiliana na itikadi mbaya iliyosababisha mashambulio hayo ya London. Maimamu wa Uingereza wametoa taarifa ya pamoja itakayosomwa wakati wa sala baadaye wiki hii, wakiyalaani matendo ya kigadi.