LONDON: Ugonjwa wa miguu na midomo nchini Uingereza
22 Septemba 2007Matangazo
Kesi mpya ya ugonjwa wa miguu na midomo imethibitishwa nchini Uingereza.Maafisa wamesema, kiasi ya ngómbe 40 wamechinjwa katika shamba moja la mifugo,karibu na mji wa Egham ulio katika wilaya ya Surrey.
Majuma mawili yaliyopita,ugonjwa wa miguu na midomo ulithibitishwa katika mashamba mengine matatu katika eneo hilo la Egham.Kesi hii mpya,ni ya sita kutokea katika wilaya ya Surrey,tangu mapema mwezi wa Agosti.