LONDON: Ugonjwa wa miguu na midomo umetokea maabara
13 Septemba 2007Matangazo
Maafisa nchini Uingereza wamesema,ugonjwa wa miguu na midomo ulioripuka hivi karibuni nchini humo ni sawa na ule uliotokea mwezi uliopita. Wakulima walikuwa na wasiwasi kuwa virusi vya aina mpya vitawalazimu kuua mifugo yao.Ugonjwa wa ulioripuka mwezi uliopita kwenye shamba la mifugo katika eneo la Surrey,ulihusishwa na maabara ya jirani.