LONDON Uingereza yaahirisha msaada kwa Ethiopia
16 Juni 2005Uingereza imeahirisha nyongeza ya msaada wa kiasi cha euro milioni 45 kwa Ethiopioa, baada ya watu 36 kuuwawa katika maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi. Waziri wa maendeleo ya kimataifa, Hilary Benn, ametangaza hatua hiyo wakati wa ziara yake nchini Ethiopia. Benn amesema serikali ya Uingereza ina wasiwasi mkubwa juu ya hali hiyo nchini humo.
Watu wasiopungua 36 waliuwawa katika mji mkuu wa Addis Ababa juma lililopita wakati polisi walipowafyatulia risasi raia waliokuwa wakiandamana kupinga wizi wa kura.
Viongozi wa Ethiopia walitia sainia mkataba kufufua tena juhudi za kuyakomesha machafuko na kuanzisha uchunguzi wa malalamiko yote ya uchaguzi huo. Kiongozi wa upinzani, Hailu Shawel, aliachiliwa huru juma hili kutoka kifungo chake cha nyumbani.