1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza yapendekeza mazungumzo ya pande mbili

4 Aprili 2007

Uingereza imependekeza mazungumzo ya pande mbili kati yake na Iran kama ndio njia itakayosaidia kuutatua mzozo wa kutekwa wanamaji wake 15 katika bahari ya Shatt al Arab tangu siku kumi zilizopita.

Taarifa kutoka afisi ya waziri mkuu Tony Blair zinasema kwamba Uingereza inasubiri jibu la Iran kuhusu pendekezo hilo.

Haya yanafuatia saa chache tu tangu waziri mkuu wa Uingereza alipotamka kuwa siku mbili zijazo zitakuwa ngumu mno kabla ya mzozo huo kutatuliwa.

Wakati huo huo Tehran imeonyesha picha za wanamaji waliokamatwa wakiwa na furaha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW