1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON; Usalama kuimarika nchini Irak ?

28 Juni 2005

Waziri mkuu wa Irak bwana Ibrahim al Jafaari amesema kwamba hali ya usalama nchini Irak itaweza kuimarika katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Bwana Jafaari ameeleza matumaini hayo katika ziara yake nchini Uingereza ambapo amekutana na waziri mkuu wa nchi hiyo bwana Tony Blair.

Hatahivyo ameeleza kwamba ili kuwashinda wapinzani,majeshi ya usalama ya Irak yatapaswa kuwa na vifaa bora ,pamoja na kupatiwa mafunzo mazuri.

Bwana al Jafaari pia ametoa mwito kwa nchi zinazopakana na Irak zijaribu kuimarisha udhibiti wa mipaka yao ili kuwazuia wapiganaji kutoka nchi za nje kuingia nchini Irak.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW