London. Viongozi wakubali kuunda chombo kitakachowafuatilia Waislamu wenye imani kali.
20 Julai 2005Matangazo
Viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Uingereza , waziri mkuu Tony Blair na viongozi wa vyama vya upinzani wamekubaliana kuunda chombo maalum katika lengo la kuwafuatilia Waislamu wenye imani kali.
Haya yamekuja katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya waziri mkuu , ulioitishwa ili kujadili njia za kuliangalia tatizo lililojitokeza la mashambulizi ya mabomu dhidi ya mji wa London ambayo yameuwa watu 56 na kuwajeruhi wengine 700.
Mkutano huo umekuja siku moja baada ya Maimam wa Uingereza kutoa fatwa wakishutumu ghasia, fatwa ambayo itasomwa katika misikiti wakati wa sala wiki hii.