1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita nchini Ukraine ni changamoto kwa sekta ya anga ya Urusi

2 Julai 2023

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kuwa vita nchini Ukraine, vimekuwa changamoto ya kipekee kwa sekta ya anga ya Urusi.

MiG-29 Luftwaffe Slowakei
Picha: Petr David Josek/AP/picture alliance

Katika sasisho lake la kila siku kuhusu vita hivyo kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, wizara hiyo imesema kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto kutokana na vikwazo vya kimataifa huku wataalamu waliopata mafunzo ya juu wakihimizwa kuhudumu kama ''wanajeshi walio katika mstari wa mbele kwenye mapigano ya ardhini'' wa shirika la safari za anga la serikali ya Urusi liitwalo Roscosmos.

Mkuu wa jeshi la anga hajaonekana tangu jaribio la uasi

Wizara hiyo imesema kuwa mkuu wa vikosi vya jeshi la anga wa Urusi jenerali Sergei Surovikin, hajaonekana tangu jaribio lililotibuka la uasi lililofanywa na kundi la mamluki la Wagner ambapo alihudumu kama chanzo cha mawasiliano kati ya vikosi hivyo na wizara ya ulinzi ya Urusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW