1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Wakimbizi wagoma kula chakula

26 Juni 2005

Serikali ya Uingereza inaendelea kushinikizwa kuwa iache kuwafukuza Wazimbabwe waliokosa kupata hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza.Miongoni mwa Wazimbabwe 116 wanaongojea kurejeshwa nyumbani,41 wamegoma kula.Kampeni ya kuishinikiza serikali ya Uingereza hasa inahusika na kisa cha Crespen Kulingi aliekuwa mtayarishaji wa uchaguzi katika chama kikuu cha upinzani MDC,nchini Zimbabwe. Kulingi amesema,aliondoka Zimbabwe Septemba mwaka jana,baada ya kushambuliwa na wanajeshi.Katika kipindi cha miaka minne,ikiwa ni hadi mwaka 2004,zaidi ya Wazimbabwe 15,000 walikimbilia Uingereza.Ni mia kadhaa tu waliopewa hifadhi ya kisiasa.Hadi wakimbizi 95 walirejeshwa Zimbabwe katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW