LONDON : Wanamuziki watuma ujumbe duniani kuhusu umaskini Afrika
3 Julai 2005Maonyesho ya muziki jukwaani yaliopewa jina la Live 8 ambayo ni makubwa kabisa kuwahi kufanyika yamepeleka ujumbe wa muziki na wa kisiasa duniani kote hapo jana kwa lengo la kuyashinikiza mataifa yenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani kukomesha umaskini barani Afrika.
Zaidi ya watu milioni moja walikusanyika miongoni mwa miji mengine London,Philadelphia, Berlin,Tokyo,Paris na Johannesburg kuhudhuria maonyesho hayo ya wanamuziki mashuhuri jukwaani yaliyoandaliwa na mwanamuziki wa Ireland Bob Geldof ambaye amewataka mashabiki 200,000 waliohudhuria maonyesho ya London kutowa kilio chao kwa viongozi wa kundi la mataifa manane yenye maendeleo ya viwanda duniani wanaokutana Scotland wiki ijayo kuacha kutowa vizingizio zaidi.
Geldof amesema kwenye uwanja wa Hayde Park kwamba Mahatma Ghandhi amelikombowa bara.Martin Lurther King amewakombowa watu,Nelson Mandela ameikombowa nchi kwa hiyo inawezekana na viongozi hao wa mataifa tajiri wawatasikiliza.
Geldof aliandaa maonyesho ya muziki ya kutafuta msaada hapo mwaka 1985 ambayo yalichangisha dola milioni 100 kwa ajili ya wananchi wa Ethiopia waliokuwa wakifa njaa.