LONDON: Waziri mkuu wa Uingereza atangaza tarehe ya uchaguzi.
6 Aprili 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ametangaza kuwa uchaguzi mkuu nchini Uingereza utafanyika tarehe 5.05.05.
Ijapokuwa Tony Blair atatetea kipindi cha tatu kwa tikiti ya chama chake cha Labour wadadisi wanasema kuwa upinzani utakuwa mkali.
Kura ya maoni nchini Uingereza inaonyesha kuwa chama cha Labour kinaongoza kwa asilimia chache dhidi ya chama cha Conservative, nafasi ya tatu inakwenda kwa chama cha Liberal Democratic.
Serikali ya Uingereza sasa inahitajika kupitisha vipengele vya sheria vilivyosalia kabla ya bunge kuvujnwa kwa ajili ya kampeini za uchaguzi.