LONDON: Waziri Mkuu wa Uingereza ziarani Marekani
29 Julai 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown amesisitiza uhusiano wa karibu kati ya nchi yake na Marekani. Ametamka hayo,kabla ya kuanza ziara yake ya kwanza nchini Marekani,tangu kushika wadhifa mpya mwezi uliopita.Katika taarifa iliyotolewa,Waziri Mkuu Brown alisema,mafungamano na Marekani yapaswa kuwa uhusiano wa pande mbili ulio muhimu kabisa.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya hapo awali afisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Brown kusema kuwa katika sera za kigeni,Uingereza haitogandama tena na Marekani.
Waziri Mkuu Brown anaelekea Marekani na atakutana na Rais Bush kabla ya kwenda New York kuhotubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.