1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON.Bomu lililotegwa kwenye barua lalipuka, mmoja ajeruhiwa

5 Februari 2007

Bomu lililotegwa ndani ya barua limelipuka na kumjeruhi mwanamke mmoja katika ofisi moja katikati ya mji wa London.

Mwanamke huyo amelazwa katika hospitali moja mjini humo.

Polisi wamesema kwamba eneo la barabara ya Victoria katikati ya mji wa London liliwekwa chini ya ulinzi baada ya kupokea taarifa za tahadhari kuhusu kifurushi kilichoshukiwa.

Polisi wa kupambana na ugaidi wa kikosi cha Scotland Yard wanaendesha uchunguzi.