1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Huenda Uingereza ikaitia katika hali ngumu katiba ya Umoja wa Ulaya

6 Juni 2005

Msemaji wa serikali ya Uingereza amesema nchi hiyo inatarajiwa kuitumbukiza katiba mpya ya Umoja wa Ulaya katika hali ngumu baada ya kukataliwa na wafaransa na waholanzi.

Msemaji wa bwana Tony Blair amesema kwamba waziri wa mambo ya kigeni bwana Jack Straw atatoa taarifa ya serikali kuhusu katiba hiyo hii leo katika bunge la nchi hiyo.

Hata hivyo kulingana na sheria za bunge alikataa kutoa maelezo zaidi kuhusiana na taarifa hiyo.Matokeo ya kura ya maoni yanaonyesha kuungwa mkono kwa katiba hiyo ya Umoja wa Ulaya kumepungua huko nchini Denmark,Ureno,Poland na jamhuri ya Chek kufuatia hatua iliyochukuliwa na Ufaransa na Uholanzi.

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schoeder na rais wa Ufaransa Jacque Chiraq wamesisitiza kwamba harakati za kuiidhinisha katiba hiyo lazima ziendelee katika mataifa yote wanachama wa umoja huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW