1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Mkutano wa viongozi wa EU wafanyika London.

27 Oktoba 2005

Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana mjini London hivi sasa kwa mkutano wao usio wa kawaida.Viongozi hao ambao ni marais pamoja na wakuu wa serikali kutoka mataifa 25 ya Ulaya,wanatazamiwa kuchunguza kwa makini athari za utandawazi kwa Umoja wa Ulaya.

Jana Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair,ambaye kwa sasa anashikilia Urais wa Umoja wa Ulaya, aliliarifu Bunge la Ulaya huko Strasbourg kwamba,Umoja huo unahitaji kuwa na mwelekeo mpya wa kiuchumi,iwapo utahitaji kukabiliana na changamoto za utandawazi.

Bwana Blair pia alieleza kuwa amegundua maeneo kadhaa muhimu yatakayosaidia Umoja wa Ulaya kuongeza pato ikiwa na sekta ya utafiti,elimu na uhamiaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW