1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Uingereza yatangaza hatua za kupambana na Waislamu wenye msimamo mkali.

24 Agosti 2005

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza,Charles Clarke,ametangaza hatua mpya zenye lengo la kupambana na vikundi vya Waislamu wenye itikadi kali,kufuatia mashambulio ya mabomu ya mwezi uliopita mjini London.

Bwana Clarke ametoa orodha ya vitendo visivyokubalika,ambayo inamlenga mtu yeyote asiye raia wa Uingereza anaeishi Uingereza ama nje ya nchi hiyo,ambaye atakabiliwa na hatari ya kutimuliwa nchini Uingereza au kupigwa marufuku kuingia nchini humo.

Orodha ya vitendo hivyo vinajumuisha hatua ya mtu kuelezea hisia zake,ambazo zitaonekana zinachochea vitendo vya ugaidi,ambavyo baadae vinaweza kuwashawishi wengine kufanya vitendo vya kigaidi.

Waziri Clarke amesisitiza hata hivyo,kuwa orodha hiyo haikukusudiwa kuzima uhuru wa kujieleza,licha ya vikundi vya kutetea haki za binadamu kuonesha inaweza kuelekea huko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW