1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lori ya mafuta yalipuka Uganda na kuwauwa watu 11

23 Oktoba 2024

Watu 11 wakiwemo watoto wawili wamekufa nchini Uganda, baada ya lori la mafuta kupata ajali na kisha kulipuka.

Kenya | Mlipuko wa lori la lori mjini Kisumu
Watu walisimama karibu na lori la mafuta lililoteketea na kuwaka moto lilipopinduka magharibi mwa Kenya, huku umati ukiwa umejazana kujikingia mafuta yaliyokuwa yakimwagika, Kaskazini magharibi mwa Nairobi, kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi kati ya Kisumu na mpaka na Uganda, Julai 18 2021 Picha: AFP/Getty Images

Polisi wamesema ajali hiyo ilitokea mida ya saa tisa alasiri hapo jana katika mji wa Kigogwa, takriban kilometa 25 kaskazini mwa mji mkuu Kampala. Taarifa ya Polisi imeongeza kuwa baadhi ya miili iliharibiwa na moto kiasi cha kutotambulika huku majengo manne yakiteketezwa pia na moto huo. Lori hiyo ililikuwa ikisafiri kutoka Kampala kwenda Gulu kaskazini mwa Uganda, ambayo ni safari ya takriban kilomita 650. Katika miaka ya hivi karibuni, Uganda imeshuhudia matukio kadhaa kama hayo ambapo watu hukimbilia kuchota mafuta kutoka kwa lori zilizopata ajali. Haya yanajiri wakati mnamo Oktoba 15, lori la mafuta liliripuka kaskazini mwa Nigeria na kuua zaidi ya watu 170.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW