1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LOS ANGELES : Wanajeshi 14 wa Chile wauwawa na dhoruba ya theluji

21 Mei 2005

Takriban wanajeshi 14 wa Chile wamekufa kutokana na kuganda na theluji wakati wa mazoezi ya kijeshi mlimani ambayo yalikumbwa na dhoruba ya theluji.

Wanajeshi wengine 27 bado hawajulikani walipo na inahofiwa kuwa wamekufa baada kuwepo mlimani kwa siku tatu. Rais Ricardo Lagos wa Chile ametangaza kuongezeka kwa idadi hiyo ya vifo ambapo awali ilikuwa watu watano na ametangaza siku tatu za maombolezo ya taifa.

Jemedari Mkuu wa Majeshi Juan Cheyre amelaumu maafisa wa kijeshi kwa maafa hayo ambao waliwaamuru mamia ya wanajeshi kuondoka katika sehemu za kujihifadhi na kutoka nje wakati wa dhoruba hiyo ya theluji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW