JamiiMarekani
Los Angeles yachunguza mapungufu ya kubaliana na moto mkali
11 Januari 2025Matangazo
Gavana wa California, Gavin Newsom, ameomba kufanyika uchunguzi huru katika Idara ya maji na umeme ya mji wa Los Angeles. Uchunguzi unahusu uhaba wa maji kwenye idara ya wazimamoto huku wakikabiliana na moto mkali unaoteketeza makaazi na miundombinu ya mji huo wa kifahari wa Marekani.
Gavana Newsom amesema ripoti za mapungufu ya maji na ukosefu wa usambazaji wa maji kwenye hifadhi muhimu "zinasumbua sana."
Alisema uhaba wa usambazaji wa maji kwa mabomba ya maji "huenda ukadhoofisha juhudi za kulinda baadhi ya nyumba na njia za uokoaji."
Mamlaka nchini Marekani zimetangaza amri ya kutotembea nje katika maeneo ya Los Angeles, ambako jumla ya watu 10 wamekufa kufikia sasa kutokana na moto huo.