LUANDA : Gonjwa thakili kama Ebola lauwa 4
27 Machi 2005Matangazo
Nchini Angola watu wanne imeripotiwa kuwa wamekufa kutokana na gonjwa thakili la virusi vya Marbug katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
Tokea mwezi wa Oktoba mwaka 2004 watu 120 wamekufa nchini Angola kutokana na gonjwa hilo ambalo linafanana na lile la virusi vya Ebola la homa ya kuvuja damu ambalo mlipuko wake katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo uliuuwa watu 123 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2000.
Wataalamu bingwa 30 kutoka Shirika la Afya Duniani na makundi mengine hivi sasa wanakimbilia kaskazini mwa Angola katika jitihada za kuzuwiya kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa huo ambao tiba yake haijulikani.