LUANDA: Huduma za tiba zimeshitishwa na WHO
10 Aprili 2005Matangazo
Shirika la Afya Duniani-WHO la Umoja wa Mataifa limesitisha huduma za kujaribu kuzuia mripuko wa virusi vya Marburg,magharibi mwa Angola.Siku ya Alkhamis wakaazi wa sehemu hiyo waliwashambulia maafisa wa tiba wa WHO,ikisemekana kuwa wanaamini watumishi hao ndio wamepeleka virusi hivyo katika eneo hilo.Tangu mwezi wa Oktoba,mripuko wa virusi vya Marburg umesababisha si chini ya vifo 183.Hakuna chanjo au matibabu yanayojulikana kwa virusi hivyo.